10 Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu,wamelikanyagakanyaga chini lililo mali yangu;shamba langu zuri wamelifanya jangwa.
11 Wamelifanya kuwa tupu;katika ukiwa wake lanililia.Nchi yote imekuwa jangwa,wala hakuna mtu anayejali.
12 Juu ya milima yote jangwani,watu wamefika kuangamiza.Upanga wangu unapita kuiangamiza nchi,toka upande mmoja hadi mwingine,wala hakuna mtu atakayeishi kwa amani.
13 Walipanda ngano, lakini walivuna magugu;walifanya bidii, lakini hawakupata kitu.Kwa sababu ya hasira yangu kali,mavuno watakayoyapata yatakuwa aibu tupu.”
14 Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya jirani wabaya wa watu wangu: “Wamekigusa kile kilicho changu, kile nilichowapa watu wangu Israeli! Basi nitawangoa kutoka katika nchi yao. Hata watu wa Yuda nitawangoa katika nchi yao.
15 Lakini baada ya kuwangoa, nitawahurumia tena; nitalirudisha kila taifa katika sehemu yake na katika nchi yake.
16 Na kama watajifunza njia za watu wangu kwa moyo wote, kama wataapa kwa jina langu kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu,’ kama vile walivyowafundisha watu wangu kuapa kwa jina la mungu Baali, basi watajengeka miongoni mwa watu wangu.