18 Mwambie mfalme na mama yake hivi:“Shukeni kwenye viti vyenu vya enzi,maana taji zenu nzuri zimeanguka vichwani mwenu.
19 Miji ya Negebu imezingirwa;hakuna awezaye kufungua malango yake.Watu wa Yuda wamechukuliwa mateka,wote kabisa wamepelekwa utumwani.”
20 Inua macho yako, ee Yerusalemu!Tazama! Madui zako waja kutoka kaskazini.Kundi ulilokabidhiwa liko wapi?Kundi lako zuri li wapi?
21 Utasemaje juu ya wale uliodhani ni rafiki,wale ambao wewe mwenyewe uliwafundisha,watakapokushinda na kukutawala?Je, si utakumbwa na uchungukama wa mama anayejifungua?
22 Nawe utajiuliza moyoni mwako,“Kwa nini mambo haya yamenipata?”Sawa! Kama vazi lako limepandishwa juu,nawe ukatendewa kwa ukatili mno,hayo ni matokeo ya makosa yako mengi mno.
23 Je, Mwethiopia aweza kubadili rangi yake,au chui madoadoa yake?Ikiwezekana, nanyi pia mnaweza kutenda mema,nyinyi mliozoea kutenda maovu!
24 Mwenyezi-Mungu atawatawanya kama makapiyanayopeperushwa na upepo kutoka jangwani.