5 Lakini kama hamtatii maneno haya, mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwa nafsi yangu kwamba mahali hapa patakuwa magofu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
6 Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu ikulu ya mfalme wa Yuda:“Ingawa waonekana kuwa mzuri kama nchi ya Gileadikama kilele cha Lebanoni,Lakini naapa kuwa nitakufanya uwe jangwa,uwe mji usiokaliwa na watu.
7 Nitawatayarisha waangamizi dhidi yako,kila mmoja na silaha yake mkononi.Wataikata mierezi yako mizuri,na kuitumbukiza motoni.
8 “Kisha watu wengi wa mataifa watapita karibu na mji huu, na kila mmoja atamwuliza mwenzake: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameutenda hivi mji huu mkubwa?’
9 Wenzao watawajibu, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaiabudu miungu mingine na kuitumikia.’”
10 Msimlilie mtu aliyekufa,wala msiombolezee kifo chake.Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.
11 Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Shalumu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyetawala baada ya Yosia baba yake, na ambaye aliondoka mahali hapa: “Shalumu hatarudi tena mahali hapa,