7 Nitawatayarisha waangamizi dhidi yako,kila mmoja na silaha yake mkononi.Wataikata mierezi yako mizuri,na kuitumbukiza motoni.
8 “Kisha watu wengi wa mataifa watapita karibu na mji huu, na kila mmoja atamwuliza mwenzake: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameutenda hivi mji huu mkubwa?’
9 Wenzao watawajibu, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaiabudu miungu mingine na kuitumikia.’”
10 Msimlilie mtu aliyekufa,wala msiombolezee kifo chake.Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.
11 Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Shalumu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyetawala baada ya Yosia baba yake, na ambaye aliondoka mahali hapa: “Shalumu hatarudi tena mahali hapa,
12 bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii.
13 “Ole wako Yehoyakimuwewe unayejenga nyumba kwa dhulumana kuiwekea ghorofa bila kutumia haki.Unawaajiri watu wakutumikie burewala huwalipi mishahara yao.