14 Badala yake wamefuata kwa ukaidi fikira za mioyo yao, wakaenda kuyaabudu Mabaali kama walivyofundishwa na wazee wao.
15 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Tazama nitawalisha watu hawa uchungu na kuwapa maji yenye sumu wanywe.
16 Nitawatawanya kati ya mataifa ambayo wao wenyewe wala wazee wao hawakupata kuyajua; nitawafanya waandamwe na vita mpaka hapo nitakapowaangamiza wote.”
17 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Fikirini na kuwaita wanawake waomboleze;naam, waiteni wanawake hodari wa kuomboleza.
18 Waambieni: ‘Njoni hima mkaomboleze juu yetu,macho yetu yapate kuchuruzika machozi,na kope zetu zibubujike machozi kama maji.’”
19 Kilio kinasikika Siyoni:“Tumeangamia kabisa!Tumeaibishwa kabisa!Lazima tuiache nchi yetu,maana nyumba zetu zimebomolewa!
20 Enyi wanawake, sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu!Tegeni masikio msikie jambo analosema.Wafundisheni binti zenu kuomboleza,na jirani zenu wimbo wa maziko: