2 Na wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ wewe utawajibu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Waliopangiwa kufa kwa maradhi, watakufa kwa maradhi;waliopangiwa kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga;waliopangiwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa;na waliopangiwa kuwa mateka, watatekwa mateka.
3 Mimi Mwenyezi-Mungu nimeamua kuwaletea aina nne za maangamizi: Vita itakayowaua, mbwa watakaowararua; ndege wa angani watakaowadonoa na wanyama wa porini watakaowatafuna na kuwamaliza.
4 Nitawafanya kuwa kitu cha kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu ya mambo ambayo Manase mwana wa Hezekia, aliyafanya huko Yerusalemu, alipokuwa mfalme wa Yuda.
5 “Ni nani atakayewahurumia, enyi watu wa Yerusalemu?Ni nani atakayeomboleza juu yenu?Nani atasimama kuuliza habari zenu?
6 Nyinyi mmenikataa mimi, nasema mimi Mwenyezi-Mungu;nyinyi mmeniacha mkarudi nyuma.Hivyo nimenyosha mkono kuwaangamiza,kwa kuwa nimechoka kuwahurumia.
7 Nimewapepeta kwa chombo cha kupuria,katika kila mji nchini;nimewaangamiza watu wangu,kwa kuwaulia mbali watoto wao,lakini hawakuacha njia zao.
8 Wajane wao wamekuwa wengikuliko mchanga wa bahari.Kina mama wa watoto walio vijananimewaletea mwangamizi mchana.Nimesababisha uchungu na vitishoviwapate kwa ghafla.