4 Enyi watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu,jitakaseni kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu,wekeni mioyo yenu wazi mbele yangu.La sivyo, ghadhabu yangu itachomoza kama moto,iwake hata pasiwe na mtu wa kuizima,kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
5 “Tangazeni huko Yuda,pazeni sauti huko Yerusalemu!Pigeni tarumbeta kila mahali nchini!Pazeni sauti na kusema:Kusanyikeni pamoja!Kimbilieni miji yenye ngome!
6 Twekeni bendera ya vita kuelekea Siyoni,kimbilieni usalama wenu, msisitesite!Mwenyezi-Mungu analeta maafana maangamizi makubwa kutoka kaskazini.
7 Kama simba atokavyo mafichoni mwake,mwangamizi wa mataifa ameanza kuja,anakuja kutoka mahali pake,ili kuiharibu nchi yako.Miji yako itakuwa magofu matupu,bila kukaliwa na mtu yeyote.
8 Kwa hiyo, vaa vazi la gunia,omboleza na kulia;maana, hasira kali ya Mwenyezi-Mungu,bado haijaondoka kwetu.
9 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”
10 Kisha nikasema: “Aa, Mwenyezi-Mungu, hakika umewadanganya kabisa watu hawa na mji wa Yerusalemu! Uliwaambia mambo yatawaendea vema, kumbe maisha yao yamo hatarini kabisa!”