6 Kimbieni kutoka Babuloni,kila mtu na ayaokoe maisha yake!Msiangamizwe katika adhabu yake,maana huu ndio wakati wa Mungu wa kulipa kisasi,anaiadhibu Babuloni kama inavyostahili.
7 Babuloni ilikuwa kikombe cha dhahabumkononi mwa Mwenyezi-Mungu,ambacho kiliilewesha dunia nzima.Mataifa yalikunywa divai yake,hata yakapatwa wazimu.
8 Ghafla Babuloni imeanguka na kuvunjikavunjika;ombolezeni kwa ajili yake!Leteni dawa kutuliza maumivu yake;labda utaweza kuponywa.
9 Tulijaribu kuuponya Babuloni,lakini hauwezi kuponywa.Uacheni, twendeni zetu,kila mmoja katika nchi yake,maana hukumu yake ni kuu mnoimeinuka mpaka mawinguni.
10 Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia.Twendeni Siyoni tukatangazematendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
11 Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.Noeni mishale yenu!Chukueni ngao!
12 Twekeni bendera ya vitakushambulia kuta za Babuloni.Imarisheni ulinzi;wekeni walinzi;tayarisheni mashambulizi.Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekelezamambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.