2 Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani,ambamo ningewaacha watu wangu na kwenda zangu.”Mwenyezi-Mungu asema:“Wote ni watu wazinzi,ni genge la watu wahaini.
3 Hupinda maneno yao kama pinde;wameimarika kwa uongo na si kwa haki.Huendelea kutoka uovu hata uovu,wala hawanitambui mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
4 Kila mmoja ajihadhari na jirani yake!Hata ndugu yeyote haaminiki,kila ndugu ni mdanganyifu,na kila jirani ni msengenyaji.
5 Kila mmoja humdanganya jirani yake,hakuna hata mmoja asemaye ukweli.Wamezifundisha ndimi zao kusema uongo;hutenda uovu kiasi cha kushindwa kabisa kutubu.
6 Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma,na udanganyifu juu ya udanganyifu.Wanakataa kunitambua mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
7 Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema:Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu!Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu?
8 Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu,daima haziishi kudanganya;kila mmoja huongea vema na jirani yake,lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.