7 Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema:Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu!Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu?
8 Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu,daima haziishi kudanganya;kila mmoja huongea vema na jirani yake,lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.
9 Je, nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya?Je, nisilipe kisasi kwa taifa kama hili?Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
10 Nitaililia na kuiomboleza milima;nitayaombolezea malisho nyikani,kwa sababu yamekauka kabisa,hakuna mtu apitaye mahali hapo.Hakusikiki tena sauti za ng'ombe;ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.
11 Mwenyezi-Mungu asema:“Nitaifanya Yerusalemu magofu matupu,naam, nitaifanya kuwa pango la mbweha;na miji ya Yuda nitaifanya kuwa jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu yeyote.”
12 Nami nikauliza, “Je kuna mtu mwenye hekima kiasi cha kuweza kueleza mambo haya? Mwenyezi-Mungu aliongea na nani hata huyo aweze kutangaza kitu hicho? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa tupu kama jangwa hata hakuna mtu apitaye humo?”
13 Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kwa kuwa wamekataa kushika sheria yangu niliyowapa, wamekataa kutii sauti yangu na kufuata matakwa yake.