15 Kama mimi ni mwovu, ole wangu!Kama mimi ni mwadilifu, siwezi kujisifu;kwani nimejaa fedheha, nikiyatazama mateso yangu.
16 Nikiinua kichwa tu waniwinda kama simbana kuniponda tena kwa maajabu yako.
17 Kila mara unao ushahidi dhidi yangu;waiongeza hasira yako dhidi yangu,waniletea maadui wapya wanishambulie.
18 “Ee Mungu, kwa nini ulinitoa tumboni mwa mama?Afadhali ningekufa kabla ya watu kuniona.
19 Ningepelekwa moja kwa moja kaburini,nikawa kama mtu asiyepata kuwako.
20 Je, siku za maisha yangu si chache?Niachie nipate faraja kidogo,
21 kabla ya kwenda huko ambako sitarudi,huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;