1 Kisha Yobu akajibu:
2 “Aa! Jinsi gani ulivyomsaidia asiye na uwezo!Jinsi gani ulivyomwokoa asiye na nguvu!
3 Jinsi gani ulivyomshauri asiye na hekima,na kumshirikisha ujuzi wako!
4 Lakini umetamka hayo kwa ajili ya nani?Nani aliyekusukuma kuongea hivyo?”Bildadi akajibu:
5 “Mizimu huko chini yatetemeka,maji ya chini na wakazi wake yaogopa.
6 Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu.Abadoni haina kifuniko chochote.
7 Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu,na hutundika dunia mahali pasipo na kitu,
8 huyafunga maji mawinguni yawe mazito,nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
9 Huufunika uso wa mwezina kutandaza juu yake wingu.
10 Amechora duara juu ya uso wa bahari,penye mpaka kati ya mwanga na giza.
11 Mungu akitoa sauti ya kukemea,nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu.
12 Kwa nguvu zake aliituliza bahari;kwa maarifa yake alimwangamiza dude Rahabu.
13 Kwa pumzi yake aliisafisha anga;mkono wake ulilichoma joka lirukalo.
14 Yamkini haya ni machache tu ya matendo yake,ni minongono tu tunayosikia juu yake.Nani awezaye kujua ukuu wa nguvu yake?”