1 Kisha Elihu akaendelea kusema:
2 “Je, Yobu, unaona jambo hili ni sawana kufikiri kinyume cha Mungu
3 ukiuliza: ‘Nimepata faida ganikama sikutenda dhambi?Nimefaidika kuliko kama ningalitenda dhambi?’
4 Mimi nitakujibu wewe,na rafiki zako pia.
5 Hebu zitazame mbingu!Tazama mawingu yaliyo juu kuliko wewe!
6 Ukitenda dhambi, je, Mungu ndiye unayemdhuru?Na kama ukizidisha makosa yako, wadhani unamwumiza?
7 Kama wewe ni mwema, je, unampatia faida,au yeye anapokea kitu kutoka kwako?
8 Uovu wako utamdhuru binadamu kama wewe,wema wako utamfaa binadamu mwenzako.
9 “Kwa sababu ya udhalimu mwingi watu hulia,huomba msaada kwa sababu ya mapigo ya wenye nguvu.
10 Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu, Muumba wangu,mwenye kunifanya niwe mchangamfu usiku,
11 anayetuelimisha kuliko wanyama,na kutufanya wenye hekima kuliko ndege!’
12 Watu hao huomba msaada lakini Mungu hawajibu,kwa sababu ya majivuno ya watu waovu.
13 Kweli Mungu hasikilizi kilio cha bure;Mungu Mwenye Nguvu hajali kilio hicho.
14 Atakujibu vipi wakati weweunasema kwamba humwonina kwamba kesi yako iko mbele yakena wewe unamngojea!
15 Sasa, kwa vile Mungu anazuia hasira yake,wala hajali sana makosa ya watu,
16 Yobu unafungua mdomo kusema maneno matupu,unazidisha maneno bila akili.”