Yobu 14 BHN

1 “Mtu ni mtoto tu wa mwanamke;huishi siku chache tena zilizojaa taabu.

2 Huchanua kama ua, kisha hunyauka.Hukimbia kama kivuli na kutoweka.

3 Ee Mungu, kwa nini unajali hata kumwangaliana kuanza kuhojiana naye?

4 Nani awezaye kutoa kitu kisafi kutoka kitu kichafu?Hakuna anayeweza.

5 Siku za kuishi binadamu zimepimwa;ee, Mungu umeipanga idadi ya miezi yake;hawezi kupita kikomo ulichomwekea.

6 Angalia pembeni basi, umwache;ili apate kufurahia siku zake kama kibarua.

7 Maana mti ukikatwa lipo tumaini la kuota,waweza kuchipua tena.

8 Japo mizizi yake itazeeka udongoni,na shina lake kufia ardhini,

9 lakini kwa harufu tu ya maji utachipua;utatoa matawi kama chipukizi.

10 Lakini mtu hufa na huo ndio mwisho wake.Akisha toa roho anabakiwa na nini tena?

11 “Kama vile maji yakaukavyo ziwani,na mto unavyokoma kutiririka,

12 ndivyo anavyokufa mtu, wala haamki tena;hataamka tena wala kugutuka,hata hapo mbingu zitakapotoweka.

13 “Laiti ungenificha kuzimu;ungenificha hadi ghadhabu yako ipoe;nao muda ulionipimia ukiisha ungenikumbuka.

14 Je, mtu akifa anaweza kuishi tena?Siku zangu zote za kazi ningekungojahadi wakati wa kufunguliwa ufike.

15 Hapo ungeniita, nami ningeitika,wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako.

16 Ndipo ungeweza kuzihesabu hatua zangu,ungeacha kuzichunguza dhambi zangu.

17 Makosa yangu yangefungiwa katika mfuko,nawe ungeufunika uovu wangu.

18 “Lakini milima huangukamajabali hungoka mahali pake.

19 Mtiririko wa maji hula miamba,mvua kubwa hufanya mmomonyoko wa ardhi.Ndivyo nawe unavyoharibu tumaini la binadamu.

20 Wewe wamwangusha binadamu, naye akatoweka milele;waubadilisha uso wake na kumtupilia mbali.

21 Watoto wake wakiheshimika, yeye hana habari.Wakiporomoshwa, yeye haoni kabisa.

22 Huhisi tu maumivu ya mwili wake,na kuomboleza tu hali yake mbaya.”