Yobu 36 BHN

1 Kisha Elihu akaendelea kusema:

2 “Nivumilie kidogo, nami nitakuonesha kitu;maana bado ninacho cha kusema kwa niaba ya Mungu.

3 Nitaleta hekima yangu kutoka mbali sana,na kuonesha kwamba Muumba wangu ni mwadilifu.

4 Kweli maneno yangu si ya uongo;mwenye elimu kamili yuko hapa nawe.

5 “Sikiliza Mungu ni mwenye nguvuwala hamdharau mtu yeyote;uwezo wa akili yake ni mkuu mno!

6 Hawaachi waovu waendelee kuishi;lakini huwapatia wanaodhulumiwa haki zao.

7 Haachi kuwalinda watu waadilifu;huwatawaza, wakatawala na kutukuka.

8 Lakini kama watu wamefungwa minyororo,wamenaswa katika kamba za mateso,

9 Mungu huwaonesha matendo yao maovu,na kwamba wao ni watu wenye kiburi.

10 Huwafungua masikio wasikie mafunzo,na kuwaamuru warudi na kuacha uovu.

11 Wakimtii Mungu na kumtumikia,hufanikiwa katika siku zao zote;miaka yao yote huwa ya furaha.

12 Lakini wasipomtii, huangamia kwa upanga,na kufa kwa kukosa akili.

13 “Wasiomcha Mungu hupenda kukasirika,hawamlilii msaada anapowabana.

14 Hufa wangali bado vijana,maisha yao huisha kama ya walawiti.

15 Lakini Mungu huwaokoa wanyonge kwa unyonge waohutumia shida zao kuwafumbua macho.

16 Mungu alikuvuta akakutoa taabuni,akakuweka mahali pa wasaa pasipo shida,na mezani pako akakuandalia vinono.

17 “Lakini sasa umehukumiwa kama mwovu,hukumu ya haki imekukumba.

18 Jihadhari ghadhabu isije ikakufanya ukadhihaki,au ukubwa wa mali za kukukomboa ukakupotosha.

19 Je, kilio chako kitafaa kukutoa taabuni,au nguvu zako zote zitakusaidia?

20 Usitamani usiku uje,ambapo watu hufanywa watoweke walipo.

21 Jihadhari! Usiuelekee uovumaana umepatiwa mateso kukuepusha na uovu.

22 Kumbuka ukuu wa uwezo wa Mungu;nani awezaye kumfundisha kitu?

23 Nani basi aliyeweza kumpangia njia yake,au awezaye kumwambia: ‘Umekosea?’

24 “Usisahau kuyasifu matendo yake;ambayo watu wameyashangilia.

25 Watu wote wameona aliyofanya Mungu;binadamu huyaona kutoka mbali.

26 Mungu ni mkuu mno hata hatuwezi kumjua;muda wa maisha yake hauchunguziki.

27 Yeye huyavuta kwake maji ya bahari,na kutoka ukungu hufanya matone ya mvua.

28 Huyafanya mawingu yanyeshe mvua,na kuwatiririshia binadamu kwa wingi.

29 Nani ajuaye jinsi mawingu yatandavyo,au jinsi radi ingurumavyo angani kwake?

30 Yeye huutandaza umeme wake kumzunguka,na kuvifunika vilindi vya bahari.

31 Kwa mvua huwalisha watuna kuwapatia chakula kwa wingi.

32 Huukamata umeme kwa mikono yake,kisha hulenga nao shabaha,

33 Radi hutangaza ujio wake Mungu,hata wanyama hujua kwamba anakuja.