Yobu 16 BHN

Jibu la Yobu

1 Hapo Yobu akajibu:

2 “Mambo kama hayo nimeyasikia mengi;nyinyi ni wafariji duni kabisa!

3 Mwisho wa maneno haya matupu ni lini?Au ni kitu gani kinachowachochea kujibu?

4 Kama nyinyi mngekuwa mimi, na mimi nyinyi,ningeweza kusema kama nyinyiningeweza kubuni maneno dhidi yenu,na kutikisa kichwa changu.

5 Ningeweza kuwatia moyo kwa maneno yangu,na maneno yangu ya faraja yangewatuliza.

6 “Lakini nikisema maumivu yangu hayatulii,na nikikaa kimya hayaondoki.

7 Kweli Mungu amenichakazaameharibu kila kitu karibu nami.

8 Amenifanya ninyauke, na huo ni ushindi dhidi yangu.Kukonda kwangu kumenikabilina kushuhudia dhidi yangu.

9 Amenirarua kwa hasira na kunichukia;amenisagia meno;na adui yangu ananikodolea macho.

10 Watu wananidhihaki na kunicheka;makundi kwa makundi hunizunguka,na kunipiga makofi mashavuni.

11 Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri,na kunitupa mikononi mwa waovu.

12 Nilikuwa nimestarehe, lakini akanivunjavunja,alinikaba shingo na kunipasua vipandevipande;alinifanya shabaha ya mishale yake,

13 akanipiga mishale kutoka kila upande.Amenipasua figo bila huruma,na nyongo yangu akaimwaga chini.

14 Hunivunja na kunipiga tena na tena;hunishambulia kama askari.

15 “Nimejishonea mavazi ya gunia,fahari yangu nimeibwaga mavumbini.

16 Uso wangu ni mwekundu kwa kulia,kope zangu zimekuwa nyeusi ti;

17 ingawa sijafanya dhuluma kwa mkono wangu,na sala zangu kwa Mungu ni safi.

18 “Ewe dunia, usiifunike damu yangu iliyomwagika;kilio changu kienee kila mahali.

19 Nina hakika ninaye shahidi wangu mbinguni,mwenye kunitetea yuko huko juu.

20 Rafiki zangu wanidharau;nabubujika machozi kumwomba Mungu.

21 Laiti mtu angenitetea mbele ya Mungu,kama ifanyikavyo duniani kati za watu wawili.

22 Naam, miaka yangu ni michache,nami nitakwenda huko ambako sitarudi.