1 “Mbona Mungu Mwenye Nguvu haweki wakati maalumu wa hukumu;au kwa nini wamjuao hawazijui siku hizo zake?
2 Watu wanaoondoa alama za mipaka ya mashamba,na wengine huiba mifugo na kuilisha.
3 Huwanyanganya yatima punda wao,humweka rehani ng'ombe wa mjane.
4 Huwasukuma maskini kando ya barabara;maskini wa dunia hujificha mbele yao.
5 Kwa hiyo kama pundamwitumaskini hutafuta chakula jangwaniwapate chochote cha kuwalisha watoto wao.
6 Maskini wanalazimika kuokota mabaki ya mavuno mashambani,wanaokota katika mashamba ya mizabibu ya waovu.
7 Usiku kucha hulala uchi bila nguowakati wa baridi hawana cha kujifunikia.
8 Wamelowa kwa mvua ya milimani,hujibanza miambani kujificha wasilowe.
9 Wapo na wanaowanyakua watoto yatima vifuani mwa mama yao.Wengine huwaweka rehani watoto wa maskini.
10 Watoto hao hufanywa waende uchi bila nguo,wakivuna ngano huku njaa imewabana,
11 wakiwatengenezea waovu mafuta yao,au kukamua divai bila hata kuionja.
12 Kutoka mjini kilio cha wanaokufa chasikika,na walioumizwa hupaza sauti kuomba msaada;lakini Mungu hasikilizi kabisa sala zao.
13 “Wapo wengine waovu wasiopenda mwanga,wasiozifahamu njia za mwanga,na hawapendi kuzishika njia zake.
14 Mwuaji huamka mapema alfajiri,ili kwenda kuwaua maskini na fukara,na usiku ukifika, kazi yake ni kuiba.
15 Mzinifu naye hungojea giza liingie;akisema, ‘Hakuna atakayeniona;’kisha huuficha uso wake kwa nguo.
16 Usiku wezi huvunja nyumba,lakini mchana hujifungia ndani;wala hawajui kabisa mwanga ni nini.
17 Kwao wote giza nene ni mwanga wa asubuhi;wao ni marafiki wa vitisho vya giza nene.
18 “Lakini mwasema:‘Waovu huchukuliwa haraka na mafuriko ya maji,makao yao hubaki kuwa nchi iliyolaaniwa;hakuna aendaye kwenye mashamba yao ya mizabibu.’
19 Kama theluji inavyoyeyuka katika joto na ukamendivyo Kuzimu kunavyowanyakua waovu.
20 Maana mzazi wao huwasahau watu hao,hakuna atakayewakumbuka tena.Ndivyo uovu ulivyovunjwa kama mti.
21 “Waovu huwadhulumu wanawake wasiopata watoto.Wala hawawatendei wema wanawake wajane.
22 Mungu, kwa nguvu yake huwaangamiza wenye uwezo,huinuka nao hukata tamaa ya kuishi.
23 Huwaacha waovu wajione salama,lakini macho yake huchunguza mienendo yao.
24 Waovu hufana kwa muda tu, kisha hutoweka,hunyauka na kufifia kama jani,hukatiliwa mbali kama masuke ya ngano.
25 Nani basi, awezaye kuhakikisha kuwa mimi ni mwongona kuonesha kwamba maneno yangu si kweli?”