1 Kisha Yobu akajibu:
2 “Leo pia lalamiko langu ni chungu.Napata maumivu na kusononeka.
3 Laiti ningejua mahali nitakapompata Mungu!Ningeweza kwenda hata karibu naye.
4 Ningeleta kesi yangu mbele yake,na kumtolea hoja yangu.
5 Ningeweza kujua atakachonijibu,na kuelewa atakachoniambia.
6 Je, angeshindana nami kwa nguvu zake zote?La! Bila shaka angenisikiliza.
7 Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu,Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele.
8 “Tazama, nakwenda mbele, lakini simpati,narudi nyuma, lakini siwezi kumwona.
9 Namtafuta upande wa kushoto lakini simwoni;nageukia kulia, lakini siwezi kumwona.
10 Lakini yeye anajua njia ninayofuata;atakapomaliza kunijaribunitatoka humo safi kama dhahabu.
11 Nafuata nyayo zake kwa uaminifunjia yake nimeishikilia wala sikupinda.
12 Kamwe sijaacha kushika amri yake,maneno yake nimeyatunza moyoni mwangu.
13 Lakini yeye habadiliki, nani awezaye kumgeuza?Analotaka, ndilo analofanya!
14 Atanijulisha yote aliyonipangia;na mengi kama hayo yamo akilini mwake.
15 Hivyo, natetemeka kwa hofu mbele yake;hata nikifikiria tu napatwa na woga.
16 Mungu ameufanya moyo wangu ufifie,Mungu Mwenye Nguvu amenitia hofu.
17 Maana nimekumbwa na giza,na giza nene limetanda usoni mwangu.