1 “Nimevunjika moyo, siku zangu zimekwisha,kaburi langu liko tayari.
2 Kweli wanaonidhihaki wamenizunguka,dhihaka zao naziona dhahiri.
3 “Ee Mungu, uwe mdhamini wangu mbele yako,maana hakuna mwingine wa kunidhamini.
4 Maadamu umezifumba akili za rafiki zangu;usiwaache basi wanishinde.
5 Mtu anayewasaliti rafiki zake kwa faidawatoto wake watakufa macho.
6 “Nimefanywa kuwa kichekesho kwa watunimekuwa mtu wa kutemewa mate.
7 Macho yangu yamefifia kwa uchungu;viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
8 Wanyofu wanaduwaa waonapo balaa langu,nao wasio na hatia hujichocheadhidi ya mtu wanayedhani hamchi Mungu.
9 Hata hivyo, mnyofu hushikilia msimamo wake,mtu atendaye mema huzidi kuwa na nguvu zaidi.
10 Lakini nyinyi njoni, njoni nyote tena,kwenu sitampata mwenye hekima hata mmoja.
11 “Siku zangu zimekwisha, mipango yangu imevunjwa;matazamio ya moyo wangu yametoweka.
12 Kwa hao rafiki zangu usiku ni mchana;je, ndio kusema mna mwanga gizani humu?
13 Kwa vile Kuzimu ndio nyumba yangu,na makao yangu yamo humo gizani;
14 kama naliita kaburi ‘baba yangu’na buu, ‘mama yangu’ au ‘dada yangu’,
15 je, nimebakiwa na tumaini gani?Ni nani awezaye kuona tumaini hilo?
16 Tazamio langu litashuka nami kuzimu!Tutateremka sote wawili hadi huko mavumbini!”