1 Kisha Sofari, Mnaamathi, akamjibu Yobu:
2 “Je, wingi huu wa maneno uachwe tu bila kujibiwa?Je, mtu wa maneno mengi aonesha kuwa hana hatia?
3 Je, kuropoka kwako kutanyamazisha watu?Na kama ukidhihaki, je, hamna atakayekuaibisha?
4 Wewe wadai: ‘Ninachosema ni kweli,naam, sina lawama mbele ya Mungu.’
5 Laiti Mungu angefungua kinywa chakeakatoa sauti yake kukujibu!