11 Mungu anajua watu wasiofaa;akiona maovu yeye huchukua hatua.
12 “Mpumbavu hawezi kuwa na maarifa,pundamwitu ni pundamwitu tu.
13 “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu,utainua mikono yako kumwomba Mungu!
14 Kama una uovu, utupilie mbali.Usikubali ubaya uwemo nyumbani mwako.
15 Hapo utajitokeza mbele ya watu bila lawama,utakuwa thabiti bila kuwa na hofu.
16 Utazisahau taabu zako zote;utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita.
17 Maisha yako yatangaa kuliko jua la adhuhuri,giza lake litabadilika kuwa mngao wa pambazuko.