15 Hapo utajitokeza mbele ya watu bila lawama,utakuwa thabiti bila kuwa na hofu.
16 Utazisahau taabu zako zote;utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita.
17 Maisha yako yatangaa kuliko jua la adhuhuri,giza lake litabadilika kuwa mngao wa pambazuko.
18 Utakuwa na ujasiri maana lipo tumaini;utalindwa na kupumzika salama.
19 Utalala bila kuogopeshwa na mtu;watu wengi watakuomba msaada.
20 Lakini waovu macho yao yatafifia,njia zote za kutorokea zitawapotea;tumaini lao la mwisho ni kukata roho!”