5 Laiti Mungu angefungua kinywa chakeakatoa sauti yake kukujibu!
6 Angekueleza siri za hekima,maana yeye ni mwingi wa maarifa.Jua kwamba Mungu hakuhesabu makosa yako yote.
7 “Je, unaweza kugundua siri zake Munguna kujua ukomo wake yeye Mungu mwenye nguvu?
8 Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini?Kimo chake chapita Kuzimu,wewe waweza kujua nini?
9 Ukuu huo wapita marefu ya dunia,wapita mapana ya bahari.
10 Kama Mungu akipita,akamfunga mtu na kumhukumu,nani awezaye kumzuia?
11 Mungu anajua watu wasiofaa;akiona maovu yeye huchukua hatua.