8 Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini?Kimo chake chapita Kuzimu,wewe waweza kujua nini?
9 Ukuu huo wapita marefu ya dunia,wapita mapana ya bahari.
10 Kama Mungu akipita,akamfunga mtu na kumhukumu,nani awezaye kumzuia?
11 Mungu anajua watu wasiofaa;akiona maovu yeye huchukua hatua.
12 “Mpumbavu hawezi kuwa na maarifa,pundamwitu ni pundamwitu tu.
13 “Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu,utainua mikono yako kumwomba Mungu!
14 Kama una uovu, utupilie mbali.Usikubali ubaya uwemo nyumbani mwako.