12 Hekima iko kwa watu wazee,maarifa kwao walioishi muda mrefu.
13 Lakini hekima na uwezo ni vyake Mungu,yeye ana maarifa na ujuzi.
14 Akibomoa, hakuna awezaye kujenga upya;akimfunga mtu, hakuna awezaye kumfungua.
15 Akizuia mvua, twapata ukame;akiifungulia, nchi hupata mafuriko.
16 Yeye ana nguvu na hekima;wanaodanganywa na wanaodanganya ni wake.
17 Huwaacha washauri waende zao uchi,huwafanya waamuzi kuwa wapumbavu.
18 Huwavua wafalme vilemba vyao;na kuwafunga viunoni kamba za wafungwa;