21 Huwamwagia wakuu aibu,huwaondolea wenye uwezo nguvu zao.
22 Huvifunua vilindi vya giza,na kuleta mwangani yaliyokuwa gizani.
23 Huyakuza mataifa kisha huyaangamiza,huyafanya yapanuke kisha huyatawanya.
24 Huwaondolea viongozi wa watu ujuzi wao,huwafanya watangetange nyikani kusiko na njia,
25 wakapapasapapasa gizani kusiko na mwanga;na kuwafanya wapepesuke kama walevi.