1 Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:
2 “Utawinda maneno ya kusema hadi lini?Tafakari vizuri nasi tutasema.
3 Kwa nini unatufanya kama ng'ombe?Mbona unatuona sisi kuwa wapumbavu?
4 Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako.Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yakoau miamba ihamishwe toka mahali pake?
5 “Naam, mwanga wa mtu mwovu utazimishwa;mwali wa moto wake hautangaa.
6 Nyumbani kwake mwanga ni giza,taa inayomwangazia itazimwa.