11 Hofu kuu humtisha kila upande,humfuata katika kila hatua yake.
12 Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imembana;maafa yako tayari kumwangusha.
13 “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake,maradhi ya kifo hula viungo vyake.
14 Anangolewa katika nyumba aliyoitegemea,na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15 Nyumba yake tupu, wengine wataishi humo;madini ya kiberiti yametawanywa katika makao yake.
16 Yeye ni kama mti uliokauka mizizi,matawi yake juu yamenyauka.
17 Nchini hakuna atakayemkumbuka;jina lake halitatamkwa tena barabarani.