17 Nchini hakuna atakayemkumbuka;jina lake halitatamkwa tena barabarani.
18 Ameondolewa mwangani akatupwa gizani;amefukuzwa mbali kutoka duniani.
19 Hana watoto wala wajukuu;hakuna aliyesalia katika makao yake.
20 Watu wa magharibi wameshangazwa na yaliyompata,hofu imewakumba watu wa mashariki.
21 Hayo ndio yanayowapata wasiomjali Mungu;hapo ndipo mahali pa wasiomjua Mungu.”