5 “Naam, mwanga wa mtu mwovu utazimishwa;mwali wa moto wake hautangaa.
6 Nyumbani kwake mwanga ni giza,taa inayomwangazia itazimwa.
7 Hatua zake ndefu zitafupishwa;mipango yake itamwangusha chini.
8 Nyayo zake mwenyewe zitamtia mtegoni;kila akitembea anakumbana na shimo.
9 Mtego humkamata kisiginoni,tanzi humbana kabisa.
10 Amefichiwa kitanzi ardhini;ametegewa mtego njiani mwake.
11 Hofu kuu humtisha kila upande,humfuata katika kila hatua yake.