7 Hatua zake ndefu zitafupishwa;mipango yake itamwangusha chini.
8 Nyayo zake mwenyewe zitamtia mtegoni;kila akitembea anakumbana na shimo.
9 Mtego humkamata kisiginoni,tanzi humbana kabisa.
10 Amefichiwa kitanzi ardhini;ametegewa mtego njiani mwake.
11 Hofu kuu humtisha kila upande,humfuata katika kila hatua yake.
12 Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imembana;maafa yako tayari kumwangusha.
13 “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake,maradhi ya kifo hula viungo vyake.