1 Kisha Yobu akajibu:
2 “Mtaendelea kunitesa mpaka lini,na kunivunjavunja kwa maneno?
3 Mara hizi zote kumi mmenishutumu.Je, hamwoni aibu kunitendea vibaya?
4 Hata kama ingekuwa nimekosa kweli,kosa langu lanihusu mimi mwenyewe.
5 Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza;mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu.
6 Jueni kwamba Mungu amenitendea vibaya,na kuninasa katika wavu wake.