13 Mungu amewaweka ndugu zangu mbali nami;rafiki zangu wakuu wamenitoroka kabisa.
14 Jamaa zangu na marafiki hawanisaidii tena.
15 Wageni nyumbani mwangu wamenisahau;watumishi wangu wa kike waniona kuwa mgeni.Mimi nimekuwa kwao mtu wasiyemjua.
16 Namwita mtumishi wangu lakini haitikii,ninalazimika kumsihi sana kwa maneno.
17 Nimekuwa kinyaa kwa mke wangu;chukizo kwa ndugu zangu mwenyewe.
18 Hata watoto wadogo hunidharau,mara ninapojitokeza wao hunizomea.
19 “Rafiki zangu wakuu wanachukizwa nami,wale niliokuwa nikiwapenda wamenipa kisogo.