14 Jamaa zangu na marafiki hawanisaidii tena.
15 Wageni nyumbani mwangu wamenisahau;watumishi wangu wa kike waniona kuwa mgeni.Mimi nimekuwa kwao mtu wasiyemjua.
16 Namwita mtumishi wangu lakini haitikii,ninalazimika kumsihi sana kwa maneno.
17 Nimekuwa kinyaa kwa mke wangu;chukizo kwa ndugu zangu mwenyewe.
18 Hata watoto wadogo hunidharau,mara ninapojitokeza wao hunizomea.
19 “Rafiki zangu wakuu wanachukizwa nami,wale niliokuwa nikiwapenda wamenipa kisogo.
20 Mwili wangu umebakia tu mifupa na ngozi,nimeponea chupuchupu baada ya kupoteza yote.