17 Nimekuwa kinyaa kwa mke wangu;chukizo kwa ndugu zangu mwenyewe.
18 Hata watoto wadogo hunidharau,mara ninapojitokeza wao hunizomea.
19 “Rafiki zangu wakuu wanachukizwa nami,wale niliokuwa nikiwapenda wamenipa kisogo.
20 Mwili wangu umebakia tu mifupa na ngozi,nimeponea chupuchupu baada ya kupoteza yote.
21 Nioneeni huruma,nioneeni huruma enyi rafiki zangu;maana mkono wa Mungu umenifinya.
22 Kwa nini mnanifuatia kama Mungu?Mbona hamtosheki na mwili wangu?
23 “Laiti maneno yangu yangeandikwa!Laiti yangeandikwa kitabuni!