3 Mara hizi zote kumi mmenishutumu.Je, hamwoni aibu kunitendea vibaya?
4 Hata kama ingekuwa nimekosa kweli,kosa langu lanihusu mimi mwenyewe.
5 Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza;mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu.
6 Jueni kwamba Mungu amenitendea vibaya,na kuninasa katika wavu wake.
7 Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’Lakini sijibiwi.Naita kwa sauti kubwa,lakini sipati haki yangu.
8 Njia yangu ameiziba kwa ukuta ili nisipiteamezitia giza njia zangu.
9 Amenivua fahari yangu;ameiondoa taji yangu kichwani.