7 Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’Lakini sijibiwi.Naita kwa sauti kubwa,lakini sipati haki yangu.
8 Njia yangu ameiziba kwa ukuta ili nisipiteamezitia giza njia zangu.
9 Amenivua fahari yangu;ameiondoa taji yangu kichwani.
10 Amenivunja pande zote, nami nimekwisha;tumaini langu amelingoa kama mti.
11 Ameichochea ghadhabu yake dhidi yangu;ameniona kuwa kama adui yake.
12 Majeshi yake yanijia kwa pamoja;yametengeneza njia ya kuja kwangu,yamepiga kambi kuizunguka nyumba yangu.
13 Mungu amewaweka ndugu zangu mbali nami;rafiki zangu wakuu wamenitoroka kabisa.