12 “Mdomoni mwake uovu ni mtamu kama sukari,anauficha chini ya ulimi wake;
13 hataki kabisa kuuachilia,bali anaushikilia kinywani mwake.
14 Lakini ufikapo tumboni huwa mchungu,mkali kama sumu ya nyoka.
15 Mwovu humeza mali haramu na kuitapika;Mungu huitoa tumboni mwake.
16 Anachonyonya mtu mwovu ni sumu ya nyoka;atauawa kwa kuumwa na nyoka.
17 Hataishi kuiona mitiririko ya fanaka,wala vijito vya mafanikio na utajiri.
18 Matunda ya jasho lake atayaachilia,hatakuwa na uwezo wa kuyaonja,