20 “Kwa vile ulafi wake hauna mwisho,hataweza kuokoa chochote anachothamini.
21 Baada ya kula hakuacha hata makombo,kwa hiyo fanaka yake yote haitadumu.
22 Kileleni mwa fanaka dhiki itamvamia,balaa itamkumba kwa nguvu zote.
23 Akiwa anajishughulisha kushibisha tumbo,Mungu atamletea ghadhabu yakeimtiririkie kama chakula chake.
24 Labda ataweza kuepa upanga wa chuma,kumbe atachomwa na upanga wa shaba.
25 Mshale utachomolewa kutoka mwilini mwake;ncha yake itatolewa mgongoni mwake ikingaa,vitisho vya kifo vitamvamia.
26 Hazina zake zitaharibiwa,moto wa ajabu utamteketeza;kilichobaki nyumbani mwake kitateketezwa.