3 Nasikia maonyo nisiyoweza kuvumilia,lakini akili yangu yanisukuma nijibu.
4 “Wewe labda umesahau jambo hili:Kwamba tangu zamani Mungu alipomuumba mtu duniani,
5 mwovu atajiona ameshinda kwa muda tu,furaha yake asiyemcha Mungu ni ya muda mfupi tu!
6 Mwovu aweza kufana hata kufikia mbingu,kichwa chake kikafika kwenye mawingu,
7 lakini atatupiliwa mbali kama mavi yake.Waliopata kumjua watajiuliza: ‘Yuko wapi?’
8 Atatoweka kama ndoto, asionekane tena,atafutika kama maono ya usiku.
9 Aliyemwona, hatamwona tena,wala pale alipoishi hapatatambuliwa tena.