17 “Mara ngapi umepata kuona mwanga wa maisha ya mwovu umezimwa,wakapata kukumbwa na maafa,au Mungu amewahi kuwaangamiza kwa hasira yake?
18 Hata hivyo, na wapeperushwe kama majani makavu,wawe kama makapi yanayochukuliwa na dhoruba!
19 “Nyinyi mwasema, ‘Mungu amewawekea watoto waoadhabu ya watu hao waovu.’Kwa nini hawalipizi wao wenyewe, wapate kutambua!
20 Waone wao wenyewe wakiangamia;waone wenyewe ghadhabu ya Mungu mwenye nguvu.
21 Maana wakifa watajali nini juu ya wazawa wao,wakati siku zao zitakapokuwa zimefika mwisho?
22 Je, binadamu aweza kumfunza Mungu maarifa,Mungu ambaye huwahukumu wakazi wa mbinguni?
23 “Mtu hufa katika kilele cha ufanisi wake,akiwa katika raha mustarehe na salama;