21 Maana wakifa watajali nini juu ya wazawa wao,wakati siku zao zitakapokuwa zimefika mwisho?
22 Je, binadamu aweza kumfunza Mungu maarifa,Mungu ambaye huwahukumu wakazi wa mbinguni?
23 “Mtu hufa katika kilele cha ufanisi wake,akiwa katika raha mustarehe na salama;
24 amejaa mafuta tele mwilini,na mifupa yake ikiwa bado na nguvu.
25 Mwingine hufa na huzuni kubwa moyoni,akiwa hajawahi kuonja lolote jema.
26 Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa,wote hufunikwa na mabuu.
27 “Sikilizeni! Mimi nayajua mawazo yenu yote,na mipango yenu ya kunidharau.