30 Mwovu husalimishwa siku ya maafa,huokolewa siku ya ghadhabu!
31 Ni nani atakayemshutumu mtu mwovu,au atakayemlipa kwa yote aliyotenda?
32 Anapochukuliwa kupelekwa kaburini,kaburi lake huwekewa ulinzi.
33 Watu wengi humfuata nyumana wengine wengi sana humtangulia.Anapozikwa, udongo huteremshwa taratibu.
34 Mtawezaje basi, kunifariji kwa maneno matupu?majibu yenu hayana chochote ila uongo.”