8 Huwaona watoto wao wakifanikiwa;na wazawa wao wakipata nguvu.
9 Kwao kila kitu ni salama bila hofu;wala kiboko cha Mungu hakiwafikii.
10 Naam, ng'ombe wao wote huongezeka,huzaa bila matatizo yoyote.
11 Watoto wao wachanga huwatembeza kama kundi;na watoto wao hucheza ngoma;
12 hucheza muziki wa ngoma na vinubi,na kufurahia sauti ya filimbi.
13 Huishi maisha ya fanakakisha hushuka kwa amani kuzimu.
14 Humwambia Mungu, ‘Usitusumbue!Hatutaki kujua matakwa yako.