1 Kisha Yobu akajibu:
2 “Aa! Jinsi gani ulivyomsaidia asiye na uwezo!Jinsi gani ulivyomwokoa asiye na nguvu!
3 Jinsi gani ulivyomshauri asiye na hekima,na kumshirikisha ujuzi wako!
4 Lakini umetamka hayo kwa ajili ya nani?Nani aliyekusukuma kuongea hivyo?”Bildadi akajibu:
5 “Mizimu huko chini yatetemeka,maji ya chini na wakazi wake yaogopa.
6 Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu.Abadoni haina kifuniko chochote.
7 Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu,na hutundika dunia mahali pasipo na kitu,