1 Yobu akaendelea kutoa hoja yake, akasema:
2 “Naapa kwa Mungu aliye hai,aliyeniondolea haki yangu,Mungu Mwenye Nguvu aliyeifanya nafsi yangu iwe na uchungu!
3 Naapa kuwa kadiri ninavyoweza kupumua,roho ya Mungu ikiwa bado ndani yangu;
4 midomo yangu kamwe haitatamka uongo,wala ulimi wangu kusema udanganyifu.
5 Siwezi kabisa kusema kuwa nyinyi mnasema ukwelimpaka kufa kwangu nasema sina hatia.
6 Nashikilia unyofu wangu, wala sitauacha;katika dhamiri yangu sina cha kunihukumu maishani mwangu.