11 Nitawafundisheni kitendo cha Mungu kilivyo,sitawaficheni mipango yake Mungu Mwenye Nguvu.
12 Lakini nyinyi mnajua jambo hilo vizuri sana!Mbona, basi mnaongea upuuzi?
13 “Hiki ndicho Mungu alichomwekea mtu mwovu,alichopangiwa mdhalimu kupata ni hiki:
14 Watoto wake hata wawe wengi watauawa kwa upanga;wazawa wake hawatakuwa na chakula cha kutosha.
15 Wale watakaopona watakufa kwa maradhi mabaya,na wajane wao hawatawaombolezea.
16 Hata akirundika fedha kama mavumbi,na mavazi kama udongo wa mfinyanzi,
17 na arundike tu, lakini mnyofu ndiye atakayeyavaa,na fedha yake watagawana watu wasio na hatia.