7 “Adui yangu na apate adhabu ya mwovu,anayeinuka kunilaumu aadhibiwe kama mbaya.
8 Asiyemcha Mungu ana tumaini gani,Mungu anapomkatilia mbali,anapomwondolea uhai wake?
9 Je, atakapokumbwa na taabu,Mungu atasikia kilio chake?
10 Mwovu hawezi kufurahi mbele ya Mungu Mwenye Nguvu;hataweza kudumu akimwomba Mungu.
11 Nitawafundisheni kitendo cha Mungu kilivyo,sitawaficheni mipango yake Mungu Mwenye Nguvu.
12 Lakini nyinyi mnajua jambo hilo vizuri sana!Mbona, basi mnaongea upuuzi?
13 “Hiki ndicho Mungu alichomwekea mtu mwovu,alichopangiwa mdhalimu kupata ni hiki: