12 Nilimwokoa maskini aliyenililia msaada,kadhalika na yatima asiyekuwa na wa kumsaidia.
13 Waliokuwa karibu kuangamia walinitakia baraka,niliwafanya wajane waone tena furaha moyoni.
14 Uadilifu ulikuwa vazi langu;kutenda haki kulikuwa kama joho na kilemba changu.
15 Kwa vipofu nilikuwa macho ya kuwaonesha njia,kwa viwete nilikuwa miguu yao.
16 Kwa maskini nilikuwa baba yao,nilifanya bidii kutetea haki za watu nisiowajua.
17 Nilizivunja nguvu za watu waovu,nikawafanya wawaachilie mateka wao.
18 Kisha nikafikiri: Nitafia kiotani mwangu nimetulia;siku za maisha yangu zitaongezeka kama mchanga.