23 Ya nini kumjalia uhai mtu ambaye njia zake zimefungwa,mtu ambaye Mungu amemwekea kizuizi?
24 Kwa maana kusononeka ndio mkate wangu,kupiga kite kwangu kunatiririka mithili ya maji.
25 Kile ninachokiogopa kimenipata,ninachokihofia ndicho kilichonikumba.
26 Sina amani wala utulivu;sipumziki, taabu imenijia.”